TFC YAIMARISHA MAHUSIANO YA KITAASISI KATIKA SACCA CONGRESS 2026

By TFC Super Admin

TFC YAIMARISHA MAHUSIANO YA KITAASISI KATIKA SACCA CONGRESS 2026
Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania Bara (TFC) linashiriki SACCA Congress 2026 kwa lengo la kutambulisha shughuli za wanachama wake, wakiwemo wanaojishughulisha na sekta nyingine za uchumi zaidi ya ushirika wa fedha na huduma zinazotolewa na Shirikisho.

Banda la TFC limepokea wawakilishi wa Vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) kutoka nchi mbalimbali kama Ghana, Rwanda na Eswatini, walioonesha nia ya kufahamu zaidi kuhusu nafasi ya Shirikisho katika kuhudumia vyama vya ushirika vya sekta mbalimbali nchini Tanzania.

Kupitia ziara hizo, wageni wamepata fursa ya kufahamu shughuli za wanachama wa TFC, mahitaji yao na namna Shirikisho linavyowawakilisha, kutetea maslahi yao na kuratibu huduma zinazochangia maendeleo yao. Mazungumzo hayo pia yametoa nafasi ya kubadilishana uzoefu kuhusu namna vyama vya ushirika vya sekta tofauti vinavyoweza kushirikiana na kunufaishana.

Ushiriki huu unawezesha TFC kuongeza utambulisho wa wanachama wake katika ngazi ya kimataifa na kujenga mahusiano yanayoweza kufungua fursa za ushirikiano, biashara na maendeleo ya sekta ya ushirika.
Likes