TAARIFA MUHIMU KWA VYAMA VYA USHIRIKA: MAFUNZO YA MTANDAONI KUHUSU FURSA NA TARATIBU ZA UMOJA WA ULAYA (EU).

By TFC Super Admin

Kuvifanya vyama vya ushirika kuelewa jinsi ya kufanya kazi na Umoja wa Ulaya (EU), kupata fursa za ufadhili (ikiwemo mpango wa Global Gateway), na kukidhi vigezo vya usimamizi na ushirikiano.

Muungano wa Kimataifa wa Vyama vya Ushirika (ICA), kupitia ushirikiano wake na Umoja wa Ulaya (#coops4dev), umeandaa mfululizo wa mafunzo ya mtandaoni kwa njia ya Zoom kwa mwezi wa Oktoba 2026.

Lengo:
Kuvifanya vyama vya ushirika kuelewa jinsi ya kufanya kazi na Umoja wa Ulaya (EU), kupata fursa za ufadhili (ikiwemo mpango wa Global Gateway), na kukidhi vigezo vya usimamizi na ushirikiano.

Ratiba ya Mafunzo (Oktoba 2026):
1. Somo la 1 (Tarehe 7 Oktoba): Kuelewa Mfumo wa EU na Ushirikiano na Wawakilishi Wao (Understanding the EU External Action Ecosystem)
2. Somo la 2 (Tarehe 13 Oktoba): Utayari wa Vyama vya Ushirika Katika Mpango wa Global Gateway
3.Somo la 3 (Tarehe 20 Oktoba): Kuandaa Hoja Zenye Mashiko kwa Ajili ya Umoja wa Ulaya (Building a Strong Value Proposition)
4.Somo la 4 (Tarehe 29 Oktoba): Vigezo vya Uzingatiaji Sheria/Taratibu za EU na Hatua za Kuchukua (EU Compliance & Organisational Readiness)

Muda wa Mafunzo:
Kila somo litatolewa mara mbili kwa siku husika:
Asubuhi: Saa 09:30 – 12:00 CEST (Lugha ya Kiingereza)
Jioni: Saa 16:00 – 18:30 CEST (Kiingereza na Tafsiri ya Kihispania)

📌 Jinsi ya Kushiriki: Mafunzo haya ni ya bure kwa wanachama na vyama vyote vya ushirika. Unaweza kujisajili kupitia tovuti rasmi ya ICA: https://ica.coop/en/events

Tafadhali sambaza taarifa hii kwa vyama vingine vya ushirika ili visikose mafunzo haya.

"Pamoja Tujenge Uchumi"
Likes