Mameneja/watendaji wa vyama vya ushirika washiriki mafunzo ya mbinu za uandishi wa Miradi.

By TFC Super Admin

Vyama vya ushirika vina rasilimali na fursa kubwa za masoko, lakini changamoto kubwa imekuwa ni kuzibadilisha fursa hizo kuwa miradi inayowekezeka kutokana na ukosefu wa michanganuo thabiti ya biashara.

Katika kutimiza wajibu wake wa kuwajengea uwezo wanaushirika, Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) limeendesha mafunzo ya Uandishi na Usimamizi wa Miradi mkoani Arusha (17–18 Septemba 2026). Lengo kuu ni kuhamisha mtazamo kutoka kwenye maombi ya kawaida ya miradi hadi kwenye uandaaji wa maandiko yenye uchanganuzi wa kina wa tatizo, soko, gharama, mapato na mpango wa utekelezaji.

Akitilia mkazo jambo hili wakati wa kufunga mafunzo hayo, Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Arusha, Bw. Robert George, alibainisha kuwa changamoto kubwa inayokabili vyama vingi si ukosefu wa fedha au fursa, bali ni ukosefu wa maandiko bora na yenye tija yanayoweza kumshawishi mtoa fedha au mwekezaji kuwekeza. Bw. George ametoa shukrani na pongezi za dhati kwa uongozi wa TFC na wawezesheshaji kutoka Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) kwa kuleta mafunzo haya ya kimkakati mkoani Arusha. Alipongeza jitihada hizo za makusudi za TFC katika kuwajengea uwezo watendaji wa vyama vya Ushirika, alibainisha kuwa hatua hiyo inaonyesha wazi dhamira ya dhati ya shirikisho hilo katika kutatua changamoto za msingi za vyama vya ushirika.

Aidha, alisisitiza kuwa kumalizika kwa mafunzo haya kusiwe mwisho, bali kuwe mwanzo wa safari endelevu yenye muda maalum wa kupimana matokeo. Alihimiza kuwepo kwa utaratibu wa kufanya tathmini ili kuona ni maandiko mangapi bora yatakayowasilishwa na kutekelezwa kwa tija.

Kipimo cha ufanisi wa mafunzo haya ni kuzalishwa kwa maandiko ya miradi yanayoweza kuingia kwenye mfumo wa uwekezaji na kuunganishwa na taasisi za fedha au wadau wa maendeleo. TFC inahimiza vyama kuanzia kwenye tathmini ya rasilimali zilizopo na mahitaji halisi ili kuibua fursa zenye tija na kuongeza thamani. Mwelekeo wa TFC ni kuhakikisha mafunzo haya yanazaa maandiko thabiti, yakiwa na michanganuo ya biashara inayotekelezeka na kufikia maamuzi ya uwekezaji.

Likes