Kuwekeza kwenye Rasilimaliwatu kwa Ufanisi wa Ushirika!

By TFC Super Admin

Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) limeendesha mafunzo maalum ya kujenga uwezo watumishi wake yakilenga "Mabadiliko ya Mtazamo na Utamaduni katika Taasisi" (Mindset and Cultural Change for Organizations).

Kuwekeza kwenye Rasilimaliwatu kwa Ufanisi wa Ushirika!
Kuwekeza kwenye Rasilimaliwatu kwa Ufanisi wa Ushirika!
Kuwekeza kwenye Rasilimaliwatu kwa Ufanisi wa Ushirika!

​Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC) limeendesha mafunzo maalum ya kujenga uwezo watumishi wake yakilenga "Mabadiliko ya Mtazamo na Utamaduni katika Taasisi" (Mindset and Cultural Change for Organizations).

​Mafunzo haya yaliyoongozwa na mtaalamu Omary Mjenga (ndc) kutoka Centre for International Policy – Africa (CIP-Africa), yamelenga kujenga utamaduni wa kiutendaji unaojali uwajibikaji, mawasiliano ya wazi, na uongozi wenye tija.

​Kupitia mafunzo haya, timu yetu imejifunza mbinu mpya za:
✅ Kubadili mtazamo kutoka wa kusuasua kuelekea kujifunza na kuchukua hatua.
✅ Kuimarisha uwajibikaji na ushirikiano baina ya idara mbalimbali.
✅ Kuweka mipango ya utekelezaji wa siku 90 ili kuleta matokeo chanya kwa wanachama wetu.

​TFC inaamini kuwa mabadiliko endelevu ya sekta ya ushirika yanaanzia kwenye mtazamo na utamaduni bora wa kazi!
Likes